Watu 800 wauawa Gaza tangu Mei wakijaribu kupata msaada
11 Julai 2025Wengi wao waliuawa karibu na vituo vya misaada vya taasisi ya Wakfu wa Kibinadamu wa Gaza inayoungwa mkono na Marekani na Israel. Msemaji wa ofisi ya haki za binaadamu ya Umoja wa Mataifa Ravina Shamdasani amesema leo Ijumaa kwamba tangu operesheni hizo zilipoanza mwezi Mei hadi Julai 7, shirika hilo limeorodhesha "mauaji 615 karibu na maeneo ya taasisi hiyo ya misaada.
Soma pia: Amnesty International: GHF yatumika kuwauwa Wapalestina
Shamdasani amewaambia waandishi habari mjini Geneva kwamba watu wengine 183 wanadaiwa kuuawa wakati wakiwa kwenye njia za misafara ya misaada. Wakfu wa Kibinadamu wa Gaza unaoungwa mkono na Marekani na Israel ulianza operesheni zake Mei 26 baada ya Israel kusitisha usambazaji wa bidhaa katika Ukanda wa Gaza kwa zaidi ya miezi miwili, hali iliyoibua kitisho cha njaa.