Watu 60 wafa katika ajali ya boti nchini Nigeria
4 Septemba 2025Matangazo
Watu wapatao 60 wamekufa baada ya boti iliyokuwa imewabeba abiria zaidi ya 100 kupinduka katika jimbo la Niger nchini Nigeria.
Maafisa wa wilaya ya Malale wamesema, chombo hicho kiliondoka pwani ya Tungan Sule Jumanne asubuhi kuelekea Dugga ambapo abiria waliokuwemo walikuwa wanafanya ziara ya kwenda kuomboleza, wakati boti hiyo ilipogonga kisiki cha mti ndani ya maji karibu na jamii ya Gausawa katika eneo la kiserikali la Borgu.
Mtawala wa eneo hilo Abdullahi Baba Ara, amethibitisha idadi ya vifo imefikia watu 60, watu 10 wamepatikana wakiwa hai lakini wamo katika hali mahututi na wengi bado wanatafutwa.