Watu sita wameuawa katika eneo la mpaka wa Kenya na Somalia
24 Machi 2025Matangazo
Watu sita wameuawa katika shambulizi linalodaiwa kufanywa na wanamgambo wa al-Shabaab kwenye kituo cha polisi kaskazini-mashariki mwa Kenya, Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mamlaka nchini Kenya.
Wapiganaji wenye silaha waliilenga kambi hiyo ya polisi katika Kaunti ya Garissa, karibu na mpaka wa Kenya na Somalia na kufanya mauaji hayo. watu wanane walijeruhiwa. Polisi pia iliwaua washambuliaji wawili katika majibizano hayo ya risasi.
Eneo la mpakani mwa Kenya na Somalia mara nyingi hukabiliwa na mashambulizi ya wanamgambo wa Al-Shabaab, walioko kwenye eneo la nchi jirani ya Somalia.
Wanasiasa na wanaharakati wamelaani tukio hilo lakini pia wamekosoa ukandamizaji wa vikosi vya usalama kwa raia katika eneo hilo.