Watu 6 wamewaua kufuatia uvamizi na wizi wa mifugo Kenya
12 Machi 2025Matangazo
Naibu kamishna wa Samburu Kaskazini Samuel Mwangi amethibitisha tukio hilo akisema vitengo vya polisi vimerejeshwa ili kurejesha utulivu katika eneo hilo ambalo linaonekana kurudia hali ya ukosefu wa usalama.
Mwaka wa 2012 maafisa 42 wa polisi waliuawa huko Samburu eneo lililoko karibu na Baragoi wakiwa kwenye oparesheni ya kiusalama ya kukomesha uvamizi na wizi wa mifugo.
Miezi minne iliyopita Rais Ruto aliwaahidi wakaazi wa Samburu kwamba atapeleka tena Kikundi Maalum cha Operesheni ya kiusalama (SoG) katika eneo hilo, huku wenyeji wakiwa na wasiwasi wa kurejea kwa ukosefu wa usalama.