Magari na usafirishajiNigeria
Watu 6 wafariki nchini Nigeria kufuatia ajali ya lori
20 Machi 2025Matangazo
Ajali hiyo ilitokea usiku wa Jumatano kwenye barabara kuu karibu na Daraja la Nyanya huko Ayo, takriban kilomita 10 kutoka Abuja. Polisi wamesema ajali hiyo ilisababisha hofu na purukushani za madereva na raia waliokuwa wakijaribu kuondoka katika eneo hilo.
Soma pia: Mlipuko wa lori la gesi waua 140 na kujeruhi wengi Nigeria
Kutokana na ukosefu wa mfumo mzuri wa reli kwa ajili ya kusafirisha mizigo, ajali mbaya za malori hushuhudiwa mara kwa mara katika barabara kuu huko Nigeria, nchi yenye watu wengi zaidi barani Afrika.