MigogoroSudan
Watu 57 wauawa Darfur kufuatia mapigano kati ya jeshi na RSF
18 Aprili 2025Matangazo
Hayo yameelezwa jana na vyanzo mbalimbali vikisema watu hao waliuawa kufuatia mapigano ya siku ya Jumatano, huku raia wakihofia vitendo zaidi vya umwagaji damu eneo hilo wakati huu wapiganaji wakizidi kusonga mbele.
Mapigano hayo yanajiri siku chache baada ya taarifa za Umoja wa Mataifa kueleza kuwa waasi wa RSF waliwaua zaidi ya watu 400 katika mashambulizi yao huko El-Fasher , mji mkuu wa jimbo la Darfur Kaskazini na katika kambi za wakimbizi wa ndani. Mzozo huo uliotimiza miaka miwili Aprili 15, unazidi kusababisha maafa makubwa.