MigogoroSudan
Watu 5 wauawa Sudan kutokana na shambulizi la RSF Omdurman
5 Februari 2025Matangazo
Haya ni kwa mujibu wa vyanzo vya kitabibu ambavyo vimesema wahudumu wa kujitolea ni miongoni mwa waliouwawa.
Vyanzo hivyo vile vile vinaripoti kuwa mapigano yanaendelea kuzidi kote katika nchi hiyo iliyozongwa na vita.
Soma pia: Watu 40 wameuwawa baada ya RSF kushambulia soko Sudan
Hospitali hiyo ya Al-Nao ambaye inafadhiliwa na shirika la Madaktari Wasio na Mipaka MSF, iko katika eneo lililo chini ya udhibiti wa jeshi la Sudan na imeshambuliwa mara kadhaa tangu kuanza kwa vita hivyo.
Wanamgambo wa RSF wameondoka sehemu kubwa ya jimbo la kati la Al-Jazira ila wamefanya mashambulizi ya mara kwa mara katika Mji Mkuu KhaRSFrtoum na kusababisha vifo vya raia.