Janga
Watu 42 wauwawa baada ya mgodi wa dhabau kuporomoka Mali
16 Februari 2025Matangazo
Watu wengine kadhaa wamejeruhiwa katika mkasa huo.
Hii ni ajali ya pili kubwa kutokea katika taifa hilo la Magharibi mwa Afrika ambalo ni moja ya mataifa matatu ya Afrika yanayozalisha dhahabu kwa wingi.
Ajali hiyo ilitokea jana Jumamosi katika mgodi huo unaoaminika kumilikiwa na raia wa China. Muakilishi wa serikali katika mji huo amesema kwa sasa bado wanachunguza iwapo mgodi huo ulikuwa unaendeshwa kihalali.