Watu 35 hawajulikani waliko baada ya mafuriko Kherson
11 Juni 2023Matangazo
Bwawa la Kakhovka linalodhibitiwa na Urusi kwenye uwanja wa mapambano liliharibiwa Juni 6, na kusababisha maelfu ya watu kukimbia makwao na kuzusha hofu ya mzozo wa kibibinaadam pamoja na majanga ya kimazingira.
Soma pia: Urusi yadaiwa kuwashambulia watu wanaoondolewa kwenye mafuriko
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ukraine Igor Klymenko amesema miji 77 na vijiji vimefurika katika maeneo ya kusini ya Kherson na Mykolaiv.
Amesema kufuatia mafuriko hayo, watu watano wamefariki katika mkoa wa Kherson na mmoja ktika mkoa wa Mykolaiv.
Jumla ya watu 3,700 wamehamishwa kutoka makwao katika mikoa hiyo miwili. Ukraine inaituhumu Urusi kwa kulilipua bwawa hilo lililoko kwenye mto wa Dnipro, wakati Moscow ikisema Kyiv ililishambulia bwawa hilo.