Watu 34 washtakiwa juu ya mkasa wa moto Macedonia Kaskazini
13 Juni 2025Matangazo
Mwendesha mashtaka huyo wa umma Ljupco Kocevski, ameuambia mkutano wa waandishi wa habari kwamba mmiliki wa klabu, mawaziri wa zamani, mameya, wakurugenzi wa Kurugenzi ya Taifa ya Ulinzi na Uokoaji, mmiliki wa taasisi ya usalama na wanachama wake, wakaguzi wa majengo na viongozi wengine ni miongoni mwa walioshtakiwa.
Walengwa washtumiwa kwa vitendo vya uhalifu
Kocevski amesema kesi hiyo inawalenga watu 34 na taasisi 3 za kisheria kwa vitendo vya uhalifu vilivyosababisha hatari kubwa kwa maisha na mali kwa kiwango kikubwa.
Kocevski pia amesema kundi la waendesha mashtaka lilichunguza shughuli za klabu hiyo tangu kufunguliwa kwake mnamo mwaka 2012.