MigogoroMashariki ya Kati
Watu 31 wauawa Gaza kufuatia mashambulizi ya Israel
2 Septemba 2025Matangazo
Miongoni mwa waliouawa ni watu 10 katika mji wa Gaza ambapo jengo la makazi lililengwa kwa mashambulizi ya anga.
Hayo yameelezwa na Mahmoud Bassal, msemaji wa shirika la kiraia katika Ukanda huo. Israel inajiandaa kwa mashambulizi mapana zaidi ili kuchukua udhibiti wa mji wa Gaza na kuwahamisha Wapalestina karibu milioni moja, hatua inayopingwa vikali na jumuiya ya kimataifa.
Katika hatua nyingine, Ubelgiji imetangaza kuwa itaitambua Palestina kama taifa huru katika Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa . Hayo yameelezwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ubelgiji Maxime Prevot, hatua inayofuata nyayo za mataifa mengine kama Ufaransa, Canada, Uingereza na mengine, na hivyo kuzidisha shinikizo la kimataifa kwa Israel.