MigogoroSudan
Watu 30 wauawa kufuatia shambulio kwenye hospitali Sudan
25 Januari 2025Matangazo
Mashambulizi hayo ya Ijumaa jioni yalisababisha pia uharibifu mkubwa kwenye hospitali hiyo. Haijabainika wazi ni nani kati ya jeshi la Sudan na wanamgambo wa RSF aliyehusika na shambulizi hilo la droni lakini wiki iliyopita wapiganaji wa RSF waliishambulia hospitali hiyo.
Mashambulizi dhidi vituo vya afya yamekithiri huko El-Fasher , ambapo shirika la kutoa misaada la Madaktari Wasio na Mipaka MSF limesema mwezi huu kuwa hospitali hiyo ya Saudia ndiyo "hospitali pekee ya umma iliyo na uwezo wa kuendesha zoezi la upasuaji."
Takwimu rasmi zinaeleza kuwa karibu asilimia 80 ya vituo vya vya afya kote nchini Sudan vimelazimika kusitisha huduma zao kutokana na mapigano yanayoendelea.