MigogoroMashariki ya Kati
Watu 26 wauawa Gaza kufuatia mashambulizi ya Israel
19 Julai 2025Matangazo
Msemaji wa shirika la ulinzi wa raia huko Gaza Mahmud Basal amesema watu 22 wameuawa huko Khan Yunis na wanne karibu na kituo kingine kaskazini magharibi mwa mji wa Rafah.
Miito ya kufanyika mazungumzo ya kusitisha mapigano Gaza na hatimaye kuvimaliza vita hivyo imekuwa ikiongezeka, hasa wakati huu kukiripotiwa hali mbaya ya kibinadamu katika maeneo mbalimbali ya ardhi ya Palestina.