UgaidiNigeria
Watu 26 wafariki Nigeria kufuatia mripuko wa bomu
29 Aprili 2025Matangazo
Afisa wa jeshi la Nigeria ambaye hakutaka jina lake kutajwa kwa kuwa hakuwa na mamlaka ya kuzungumzia tukio hilo amesema wanaume 16, wanawake wanne na watoto sita ni miongoni mwa waliouawa, na kuongeza kuwa bomu hilo lilitegwa kando ya barabara katika kijiji cha Furunduma, karibu na mji wa Rann.
Mashambulizi ya makundi ya itikadi kali yameongezeka hivi karibuni katika jimbo la Borno ambalo ndilo chimbuko na ngome ya kundi la kigaidi la Boko Haram, ambalo uasi wake wa miaka 15, umesababisha vifo vya zaidi ya watu 40,000 na kupelekea wengine milioni mbili kuyahama makazi yao eneo hilo.