Watu 25 wauwawa katika kambi ya wakimbizi Sudan
11 Aprili 2025Matangazo
Wapiganaji wa kikosi cha Rapid Support Forces wamewaua watu 25 leo Ijumaa wakiwemo watoto na wanawake katiak shambulizi dhidi ya kambi inayokabiliwa na baa la njaa katika jimbo la Darfur Kaskazini.
Hayo yameripotiwa na wanaharakati wa kundi linalopigania demokrasia ambalo limekuwa likiratibu utoaji wa msaada kote nchini Sudan tangu vita vilipozuka kati ya jeshi na kundi la RSF mnamo Aprili 15 mwaka 2023.
Shambulizi hilo la makombora na risasi limeilenga kambi ya watu waliolazimika kuyakimbia makazi yao ya Zamzamkutokea pande mbili za kusini na mashariki.