Watu 25 wauawa katika shambulizi la anga la Israel, Gaza
22 Aprili 2025Afisa mkuu wa shirika hilo Mohammad Mughayyir, amelithibitishia shirika la habari la AFP kuhusu idadi hiyo ya waliofariki.
Mughayyir, ameongeza kuwa watu tisa waliuawa na wengine walijeruhiwa wakati shambulizi lilipoilenga nyumba moja katikati mwa mji wa kusini wa Khan Yunis. Watu sita wengine bado wamekwama chini ya vifusi.
Hamas wahimizwa wakubali mkataba ili misaada iingie Gaza
Mughayyir pia amesema watu wengine tisa wameuawa katika mashambulizi tofauti dhidi ya kambi ya wakimbizi ya Jabalia kaskazini mwa Gaza ikiwa ni pamoja na wengine watano wakati hema la watu waliopoteza makazi lilipolengwa.
Qatar yahuzunishwa na mchakato wa mazungumzo kuhusu Gaza
Jeshi la Israel halikutoa tamko la haraka kuhusu mashambulizi hayo ya hivi karibuni zaidi.Tangu kuvunjika kwa makubaliano ya kusitisha mapigano na Hamas, jeshi hilo limefanya mashambulizi makali katika Ukanda wa Gaza.