JamiiAsia
Watu 21 wafa kwa mripuko wa ghala la baruti India
2 Aprili 2025Matangazo
Vyombo vya habari vya huko vinaripoti kwamba kwenye mkasa huo uliotokea jana, watu wengine sita waliuawa.
Mratibu wa wilaya ya Banaskantha, Mihir Patel, amesema nguvu ya mripuko huo ilikuwa kubwa sana kiasi cha kuwasukuma watu umbali wa mita 300 kutoka kwenye eneo la tukio.
Majengo kadhaa yaliporomoka kwa mripuko huo, na kuwafukia watu kwenye vifusi.
Polisi inasema wengi wa walioathirika na mkasa huo ni wafanyakazi wa ghala hilo la baruti.
Matukio kama hayo yamekuwa yakitokea mara kwa mara nchini India, ambako viwango vya usalama kwa wafanyakazi ni vya chini.