Watu 20,000 wahamishwa Cologne kwa hofu ya mabomu ya zamani
4 Juni 2025Matangazo
Sehemu kubwa ya katikati mwa mji huo imefungwa ili mabomu hayo ambayo bado hayajaripuka yaweze kuteguliwa.
Vizuizi vya barabarani vimewekwa tangu saa mbili asubuhi.
Maafisa wa serikali wadumisha usalama
Maafisa wanafuatilia kuhakikisha kuwa nyumba zote zilizoko kwenye eneo la hatari katika eneo la takriban mita 1,000, ni tupu, huku msemaji mmoja wa serikali akisema kuwa inaweza kuchukua saa kadhaa kuhakikisha kuwa kila mtu ameondoka katika eneo hilo.
Waathiriwa watumai zoezi kukamilika leo
Zaidi ya watu 20,000 katika eneo hilo lililoko wilaya ya Deutz, mashariki mwa ukingo wa Mto Rhine, wameathirika na uhamishaji huo.
Kupitia ujumbe kwenye tovuti, mamlaka ya mji huo imesema kuwa kila mtu anayehusika anatumai zoezi hilo kukamilika hii ya leo.