Watu 20 wauwawa badaa ya ndege ya kivita kuanguka Bangladesh
22 Julai 2025Matangazo
Ndege ya kivita ya Bangladesh imeanguka kwenye shule moja katika mji mkuu Dhaka na kuua watu wapatao 20 na kuwajeruhi wengine zaidi ya 170, katika ajali mbaya kabisa ya usafiri wa anga kuwahi kutokea katika kipindi cha miongo kadhaa.
Wengi wa waliokufa ni wanafunzi wenye umri mdogo ambao walikuwa wameruhusiwa kutoka nje ya darasa lao wakati ndege hiyo chapa F-7 BJI iliyotengenezwa nchini China ilipoanguka katika shule hiyo ya Milestone School and College.
Taarifa ya jeshi imesema watu 20 wameuwawa, akiwemo rubani na wengine 171 wamejeruhiwa wakati ndege hiyo ilipoanguka ilipokumbwa na hitilafu ya kiufundi.