Watu 20 wauawa katika shambulizi la anga la Israel, Gaza
9 Julai 2025Matangazo
Msemaji wa shirika hilo, Mahmud Bassal, ameiambia AFP kwamba shambulio la kwanza lililenga familia moja katika eneo la Al-Mawasi, Khan Yunis, na kuua watu 10 wa familia hiyo. Shambulio la pili, lililofanyika katika kambi ya wakimbizi ya Al-Shati karibu na Gaza City, limesababisha vifo vya watu wengine 10 na kuwaacha zaidi ya 30 wakiwa wamejeruhiwa.
Qatar: Ni mapema kutarajia makubaliano ya usitishaji vita Gaza
Jeshi la Israel, kupitia taarifa kwa AFP, limesema linafanyia uchunguzi ripoti hizo.
Hata hivyo, kutokana na vikwazo vya upatikanaji wa habari na hali ngumu ya usalama katika Ukanda wa Gaza, shirika la AFP halikuweza kuthibitisha kwa njia huru idadi ya vifo na maelezo yaliyotolewa na pande zote.