Watu 20 wafariki katika kituo cha kutoa msaada Gaza
16 Julai 2025Matangazo
Katika taarifa, taasisi ya GHF imesema kuwa wahasiriwa 19 walikanyagwa hadi kufa, huku mtu mmoja akiuawa kwa kuchomwa kisu.
GHF imesema ina sababu za kuaminika kuamini kwamba washambuliaji kwenye umati wakiwa wamejihami kwa silaha na wanaohusishwa na Hamas, walichochea machafuko hayo kwa makusudi katika kituo hicho cha kusambaza misaada katikati mwa mji wa kusini wa Khan Younis.
Mashambulio mapya ya Israel yauwa Wapalestina 22 Gaza
Wafanyakazi wa GHF wanadai kuona bunduki zimebebwa na baadhi ya waliokusanyika, huku mfanyakazi mmoja wa Marekani akitishiwa kwa bunduki na mtu mmoja katika eneo hilo.
Hata hivyo madai ya shirika hilo hayajathibitishwa kwa njia huru na kundi la Hamas halijatoa tamko lolote kuhusiana na tukio hilo.