Watu 2 wauwawa na 16 kujeruhiwa Donetsk
9 Septemba 2025Raia wapatao wawili wameuliwa na wengine 16 wamejeruhiwa katika mashambulizi ya droni na makombora ya Ukraine katika maeneo yanayodhibitiwa na Urusi ya Donetsk jana Jumatatu.
Jumba la makazi la orofa tisa katika mji wa kiviwanda wa Makiivka kaskazini mwa Donetsk lililengwa na droni huku video katika mtandao wa kijamii ikionesha mashambulizi mazito ya makombora, pamoja na moja lililolenga kiwanda cha zamani cha kungenezea mifumo ya ufuatiliaji ya usalama wa anga mjini Donetsk.
Kituo kidogo karibu na mji wa Makiivka pia kimelengwa.
Mshirika ya habari ya Urusi yamewanukuu maafisa wa usalama katika maeneo yanayokaliwa wakisema droni kiasi 20 zimetumiwa katika mashambulizi mawili na vikosi vya ulinzi wa anga vimeingia kazini. Wamesema milipuko imesikika mjini Donetsk na anga la mji limegubikwa na moshi mzito.