MigogoroMashariki ya Kati
Watu 19 wauawa kufuatia mashambulizi ya Israel mji wa Gaza
5 Septemba 2025Matangazo
Kwa mujibu wa msemaji wa shirika hilo, Mahmud Bassal, ni kwamba mashambulizi ya Israel yalilenga majengo na mahema yaliyokuwa yamehifadhi watu walioyakimbia makaazi yao kutokana na mapigano yanayoendelea.
Jeshi la Israel, lilipoulizwa na shirika la habari la AFP kuhusu mashambulizi hayo, liliomba muda zaidi kuchunguza tukio hilo kabla ya kutoa maoni rasmi.
Tangu kutangazwa kwa operesheni mpya ya kijeshi mwezi uliopita, Israel imeongeza mashambulizi yake katika jiji la Gaza, ikiwa ni sehemu ya mpango wa kuliteka eneo hilo lote.
Msemaji wa jeshi la Israel, Effie Defrin, alisema jana kuwa wanajeshi wa Israel tayari wanadhibiti asilimia 40 ya jiji la Gaza.