SiasaIsrael
Watu 17 wauwawa katika mashambulizi ya Israel
4 Aprili 2025Matangazo
Miongoni mwa waliouwawa wengine ni kutoka familia moja katika mji wa kusini wa Khan Younis.
Shirika la Madaktari Wasio Mipaka , MSF, limesema mfanyakazi wake mwengine mmoja ameuawa akiwa na familia yake nzima huko Gaza.
Soma pia:UN: Mauaji ya wahudumu wa afya Gaza yanazusha wasiwasi wa "uhalifu wa kivita"
Kupitia taarifa yake, shirika hilo limesema linahuzunishwa na kufadhaishwa na mauaji ya Hussam Al-Loulou akiwa na mkewe na binti yake mwenye umri wa miaka 28.
Loulou ni mfanyakazi wa kumi na moja kuuawa tangu Israel ianzishe vita vyake kwenye Ukanda wa Gaza miezi 18 iliyopita.