Watu 15 wafariki dunia kwa Ebola Kongo
5 Septemba 2025Matangazo
Waziri wa Afya Samuel Roger Kamba amesema kwamba huo ni mripuko wa 16 wa Ebola nchini humo na kwamba kufariki kwa asilimia 53.6 ya wagonjwa kunaonyesha uzito wake.
Mwanamke mjamzito mwenye umri wa miaka 34 katika eneo la Boulape, mkoa wa Kasai Kusini ni mgonjwa wa hivi karibuni kuthibitishwa kuambukizwa Ebola.
Kwa sasa, wizara ya afya bado inaendelea kuchunguza mripuko huo.
Kamba ameelezea kuwa wagonjwa wameonyesha dalili kama vile homa, kutapika, kuharisha na kutokwa na damu nyingi.
Shirika la Afya Duniani, WHO, limesema limetuma kikosi cha wataalamu katika mkoa wa Kasai ili kuimarisha ufuatiliaji wa ugonjwa huo, matibabu na kuzuia maambukizo zaidi.