Migogoro
Watu 13 wamezama baada ya kukimbia mashambulizi Nigeria
30 Agosti 2025Matangazo
Inaarifiwa watu waliokuwa wamejazana katika boti hiyo walikuwa wanayakimbia mashambulizi ya watu waliojihami katika jimbo hilo. Maidamma Dankilo, Mkuu wa mji wa Birnin Magaji,amethibitisha mauaji ya watu hao 13.
Watu 22 wameopolewa huku wengine 22 wakiwa hawajulikani waliko.
Watu wanaodaiwa kujihami kwa silaha walikivamia kijiji cha Birnin Magaji na kuwateka nyara watu zaidi ya 100 . Katika tukio hilo watu wawili waliuwawa.
Hali hiyo ndio iliyosababisha watu wa jimbo la Zamfara kulitoroka jimbo kwa boti lililojaa watu na baadae kuzama mtoni.